No products in the cart.
Kampuni ya RABA ONE ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2015 na imekua kwa kasi kuwa moja ya kampuni zinazoongoza katika uzalishaji wa bidhaa za viwandani nchini Tanzania. Safari yetu ya mafanikio ilianza na ndoto ya kutoa bidhaa bora, salama na nafuu kwa wateja wetu.
2015: Kuanza Kwa Safari Yetu
Mwishoni mwa mwaka 2015, kampuni ya RABA ONE ilianzishwa kwa malengo makuu ya kuzalisha bidhaa za viwandani ambazo zingeleta mabadiliko makubwa kwenye soko. Ilikuwa ni kipindi cha kupanga, kutafiti na kuanzisha misingi imara ya uzalishaji.
2016: Bidhaa Yetu ya Kwanza
Mwaka 2016, tulianza rasmi uzalishaji wa bidhaa yetu ya kwanza. Ilikuwa ni hatua muhimu kwetu, kwani bidhaa hii ilipokelewa vizuri sokoni na kutupa motisha ya kuendelea mbele na uzalishaji wa bidhaa zaidi. Tangu wakati huo, tumeendelea kuboresha na kuongeza aina ya bidhaa tunazozalisha.
2018: Usajili wa Awali wa Jina la Biashara
Baada ya miaka miwili ya mafanikio na kujenga jina letu sokoni, mwaka 2018 tulipata usajili wa awali wa jina la biashara. Hii ilitupa nguvu zaidi ya kutambuliwa rasmi na kuendelea kuimarisha huduma na bidhaa zetu kwa wateja wetu.
2023: Usajili Rasmi Kama Kampuni ya Kitanzania
Mwaka 2023 ulikuwa mwaka muhimu zaidi katika historia ya RABA ONE, kwani tulipata usajili rasmi kama kampuni ya Kitanzania. Hii ilikuwa ni hatua kubwa ambayo ilithibitisha kujitolea kwetu katika kutoa bidhaa bora na huduma za hali ya juu kwa wateja wetu ndani na nje ya nchi.
Leo: Kuendelea Kupanua na Kuboresha
Leo, RABA ONE inaendelea kupanua na kuboresha bidhaa zake ambazo ni pamoja na sabuni za aina tofauti tofauti, mafuta ya kujipaka, dawa za asili za magonjwa mbalimbali, na bidhaa za nywele. Tumejikita pia katika uagizaji na usambazaji wa bidhaa zetu kwa bei nafuu, tukiwahakikishia wateja wetu ubora wa bidhaa na huduma bora.
Historia ya RABA ONE ni ushuhuda wa kujituma, ubunifu na kujitolea kwa ajili ya wateja wetu. Tunajivunia mafanikio yetu na tunaendelea kujitahidi kuwa kampuni inayoongoza katika uzalishaji wa bidhaa bora za viwandani nchini Tanzania. Tunawakaribisha wateja wetu wote waendelee kufurahia bidhaa zetu zenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu.
Sisi ni kampuni inayoongoza katika uzalishaji wa bidhaa mbali mbali za viwandani, tukijivunia ubunifu na ubora katika kila tunachofanya. Tunazingatia kutoa bidhaa bora na za kipekee zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu kwa viwango vya juu.
Bidhaa Zetu:
Tunazalisha na kusambaza bidhaa mbalimbali ambazo zimepokelewa vizuri sokoni kutokana na ubora wake wa hali ya juu. Bidhaa zetu zinajumuisha:
1. Sabuni:
– Tunazalisha sabuni za aina tofauti tofauti zinazofaa kwa matumizi ya kila siku, zenye viambato asilia na muundo wa kisasa.
2. Mafuta ya Kujipaka:
– Mafuta yetu ya kujipaka yametengenezwa kwa kutumia viambato vya asili ambavyo ni salama kwa ngozi na vina faida nyingi za kiafya, yakiwemo unyevu na ulinzi wa ngozi.
3. Dawa za Asili za Magonjwa Mbali Mbali:
– Tunatengeneza na kusambaza dawa za asili zinazosaidia katika tiba na kinga ya magonjwa mbalimbali. Dawa zetu zinatokana na mimea na viambato vya asili vilivyochaguliwa kwa uangalifu mkubwa.
4. Bidhaa za Nywele:
– Bidhaa zetu za nywele, ikijumuisha mafuta, shampoo, na conditioner, zimeundwa kusaidia katika utunzaji na ukuaji wa nywele, zikiwapa wateja wetu nywele zenye afya na nguvu.
Shughuli Zetu:
Mbali na uzalishaji wa bidhaa, tunajishughulisha pia na shughuli zifuatazo:
1. Uuzaji wa Bidhaa:
– Tunauza bidhaa zetu zote kwa bei nafuu, tukilenga kumfanya kila mteja wetu afurahie ubora kwa gharama nafuu.
2. Uagizaji wa Bidhaa Kutoka Nje ya Nchi:
– Tunajiusisha pia na uwagizaji wa bidhaa tofauti tofauti kutoka china, india, dubai, marekani na uturuki. Tunajali ubora wa bidhaa tangu mwanzo wa kuagiza hadi zinapowafikia wateja.
3. Usambazaji wa Bidhaa:
– Tunajihusisha na usambazaji wa bidhaa zetu kwa wingi ndani na nje ya nchi, tukihakikisha bidhaa zetu zinafika kwa wateja wetu popote walipo.
Hitimisho:
Tunajivunia kutoa bidhaa bora na za kipekee ambazo zinakidhi mahitaji ya wateja wetu kwa bei nafuu. Karibu ujionee tofauti ya ubora na huduma bora kutoka kwetu. Tunatumaini kuendelea kuwa mshirika wako wa kuaminika katika usafi, afya, na utunzaji wa ngozi na nywele.
Hatutoi mabadilishano lakini tunakukaribisha urudishe bidhaa/vitu vyako kwa barua kwa mujibu wa Sera yetu ya Kurejesha kwa kutumia tovuti yetu ya kurejesha bidhaa mtandaoni na kununua tena bidhaa zozote zinazopatikana kwenye tovuti yetu.
Hatutoi marejesho ya pesa taslimu. Tutakubali ubadilishanaji ndani ya siku 30 kutoka tarehe halisi ya ununuzi tukiwa na risiti halali na lebo zote zimeambatishwa. Tutakubali marejesho ya mkopo wa duka pekee ndani ya siku 30 za tarehe halisi ya ununuzi tukiwa na risiti halali na lebo zote zimeambatishwa. Bidhaa zifuatazo zinachukuliwa kuwa “Mauzo ya Mwisho” na haziwezi kubadilishwa katika duka:
Bidhaa zote zinazoisha kwa Tsh.00, .96, .97 na .98, suti za mwili, nguo za kuogelea, nguo za ndani, bidhaa za urembo, vipodozi, vifaa na “Party Wear” (kama vile mavazi ya Halloween) huchukuliwa kuwa mauzo ya mwisho, yasiyoweza kurejeshwa. na haiwezi kurejeshwa kwa mkopo wa duka.
KWENYE MSIMU HUU WA SIKUU ZA CHRISMAS NA MWAKA MPYA, JIBEBEE BIDHAA KWA BEI CHEEEE HII SIO YA KUKOSA Dismiss